![]() |
| (ndoa imeingia matatizoni sababu tu mwanamke husiliza maneno ya watu) |
karibuni sana wapenzi wafuatiliaji wa blog hii,ni kawaida yangu kuendelea kutoa ukweli unao tusaidia kujenga mauhusiano yetu huenda ya kimapenzi au ndoa,kwa dunia ya sas binadamu unapaswa kuwa makini mno katika kila jambo unalotaka kulifanya au katika maamuzi unayotaka kuyafikia,kwanini nasisitiza hivi kuna watu dunia hii wapo kama kifuata upepo hushindwa kufanya maamuzi ya msingi bali wamekuwa wakiwakabidhi watu baki waweze kuwafanyia maamuzi yanayo husiana na mustakabari wa maisha yao binafsi,watu wa namna hii hushindwa kutambua kuwa kuwa kila jambo linakua na na kmusudio lake katika maisha ya binadamu,nisikuchoshe kwa maneno yangu mengi moja kwa moja wacha nielekee katika jambo lilonifanya niwe nawe leo,USIWE SABABU MAHUSIANO KUVUNJA,hupaswi kuwa sababu ya kugombana na mpenzi wako au mume kama si mkeo
UGOMVI
katika maisha ya kawaida kabsa kukwaluzana katika maisha ya mapenzi au ndoa ni jambo la kawaida kabsaa na ukawaida wake hija pale tu mnapopishana lugha wawili nyinyi kuketi chini na kuwekana sawa,ila tu angalia na zingatia kuwa inakubidi utulie ndipo mketi kwa lengo la kutatua tatzo lenu,lakini kuna baadhii ya watu hukosea kabsa kwani huanza kuropoka maneno ya ovyoo,kashfa na matusi juu yake mtu huyu hana subira hvyo kwake kuacha au kuachwa kinaweza kikawa ni kitu cha kawaida sababu hana uvumilivu vilevile husababisha jambo dogo kuwa kubwa zaidi hatimaye hilo jambo linaweza kukosa suluhisho na kupelekea uhusiano kuvunjika au ndoa kuvunjika
USIWE MWEPESI KUAMINI
Duniani kuna watu huwa lengo lao ni kuona kina flaniwanapata shida kuhusiana na mausianao yao au ndoa zao hvyo wapo teyali kila siku kwa kazi kubwa ya kutesa mioyo ya watu makusudi kabsaa,watu hawa kila siku huja na mbinu nyingne kuona malengo yao yanatimia,ndugu yangu unapo ona kuna mtu anakuletea taarifa juu ya mpenzi wako au mume wako bila kujali kuwa ni ndugu yako wa damu au rafki yako wa kufa kuzikana unapaswa kuwa makini katika kuzipokea hzo tarifaa kabla hujanjaza utendaji,na maana kwamba usiamini moja kwa moja hyo tarifa kabla huja fanya uchunguzi yakinifu,kwani unaweza kufanya jambo ambalo kwa namna moja au nyingne likawa kero kwa mwenza wako,na kusababisha magomvi ndani ya nyumba yanayopelekea ndoia kuvunjika au uhusiano kuvunjika





