Monday, 13 June 2011

ZAWADI YA USALITI

Posted by Kitalima Gerald On 00:01
ZAWADI YA USALITI
PART 1

                                                                      Gerald kitalima-0717 199561


Janeth, Ni binti mzuri, mrembo mwenye kila aina ya mvuto machoni mwa wanaume wengi, amejawa Na maneno mazuri kinywan mwake yenye kumfaliji kila aliye pata nafasi ya kuongea nae, kutokana Na hali hiii, ilimpa wakati mgumu sanaaaaa Janeth, kwani vijana kwa wazee walihisi kupendwa na Janeth hivyo wengi wao walimuhitaji kimapenzi lakina mungu si hadhumani, hivyo Janeth aliweza kushinda majalibu yaliyo msonga kwa kufuata malengo aliyokwisha jiwekia kwambva hawezi kuingia katika suala la mapenzi na ngono  katika umri mdogo hivyo basi ukomo wa malengo yake ni pale atapofika  Elimu ya chuo kikuu na mungu atapomjalia akapata mchumba aliye mwema;amakweli nimeamini lile unalofikiri ndivyo linavyokuwa kwani malengo ya Janeth yalimfanya afanyejitiada ili  yaweze kamilika  hivyo alifaulu kidato chasita na alichaguliwa kujiunga na chuo kikuu DARES SALAAM UNIVERSITY(Mlimani)huku akitakiwa kusomea masomo ya sheria,kiukweli wazazi ,ndugu najamaa walifurahi kuona jJaneth anatimiza malengo aliyokwisha jiwekea angali bado mdogo,Mzee Masanja hakuwa  na wasi na mwanae kwani aliamini mwanae anajitambua ,anajiheshimu vilevile aliamini mwanae anajilinda kwani haijawahi tokea hata siku moja kwa mzee masanja kupata taarifa zisizo nzuri kuhusiana na Janeth; Pind janeth anasubiri ili aweze kujiunga  chuoni, nikipindi ambacho,mzee masanja alipata pesa za mafao ya uzeeni hivyo basi mambo hayakuwa mabaya kwa upande wa pesa katika familia ya mzee masanja,Baada ya miezi sita kupita Janeth alitakiwa kuwasili chuoni                                                                  

Ilikua siku ya ijumaa pale ndugu; jamaa pamoja na rafki walipokutana nyumbani kwa mzee masanja kwenye tafrija ya kumuaga bintiye Janeth, kwan siku iliyofuata alikua akielekea dar es salaam masomoni, kila mmoja alikua na furaha kwa namna yake japo wenye chuki huwahawakosekani pia vile vile wenye wivu mbaya wakiwemo ni mwiongoni mwao kutokana na mafanikio ya janeth basi bwana shamla shamla za sherehe zilipo kwisha Janeth aliwatakia usiku mwemawazazi wake kisha aliingia chumbani kwake kwa lengo la kuendelea na maandalizi ya safari kuelejea Bongo Dae es salaam,kiukweli usiku mmoja lakini kwa Janeth ulikua ni kama mwaka mzima kwani hakuweza kupata usingizi kwa muda ambao huwa anapata kila siku,usiku huu Janeth alijiuliza mambo mengi ambayo baadhi yalipata majibu lakini yaliyo mengi majibu hayakupatikana jabsa hvyo alisubiri muda yatapomkabili ndipo apambane nayo maana hakuwa na jinsi yakuyakwepa kabsaaa,janeth”Hivi nikifika Dar es salaam sina ndudu,rafki,wala mtu ninayemjua kweli nitakua na amani choni mimi?je kama nikitapeliwa nitafanyaje mimi?nikipata matatizo ugenini nani atakua teyali kunisaidia mm?” kipind Janeth akijiuliza maswali haya ndipo alipo ukalibisha usingizi bila hata kupata majibu ya maswari aliyokuwa akitafakari ,baada ya masaa kama mawili kupita  njozi juu ya malengo aliyokwisha jiwekea zilianza kumtawara binti mrembo,kwani aliota amepata mchumba anaye mjari,anamdhamini,anampenda na ameahidi kumsomesha njee ya nchii pindi atapomaliza masomo yake ya sheria ,kiukweli janeth alifurahi mnoona akamshuru mungu kumuongoza kutimiza ndoto zake na malengo yake ebwaaanaeeee Glafla Janeth anashituka usingizini anajikuta yupo kitandani,Janeth anavuta taswira anagundua kuwa alikua anaota  “Hivi mimi Janeth haya mambo naotaaa au miujizaaaaaaaa?AAAAAHHH alipigwa na butwaa kumbe ndoto ili mfanya asahau safari yake ya kuelekea dares salam hvyo alichukua saa yake ya mkononi kutizama aligundua kuwa ni saa 9 kasolo dakika 12.janeth aliona mapema mno kuanza kujiandaa kwa ajili ya safari hvyo alianza kujiuliza maana ya zile ndoto kama vile yeyen ndoo mnajimu kwakuwa hakuwa na elimu ya utabiri hvyo majibu yake ya ile ndoto yalikuwa ni mengi  kiasi kwamba alishindwa kupata maana halisi ya ndoto ile,jaeth alijipamatumaini pengine ni mpango wa mungu katika safari yake  ya maisha mapya huko aendako,akiwa katika kujiuliza maswari janeth alipitiwa na usigizi hiyvo alilala kwa mara ya pili,baada ya saa 1na nusu njozi mrembo huyo,aliota amechelewa basi stendi hvyo amekosa usafiri  kwa siku hyo na siku inayo fuata hakuna usafili uelekeao dsm alikosa raha kabsa janeth kwani alikua na wasiwasi wa kukosa nafasi chuoni kwani hajui utaratibu wa vyuo vikuu unakuwaje ikiwa katika familia ya mzee masanja yeye ndiye pekee aliyefika elimu ya chuuo kikuu,siku ya tatu basi lilifika asubuhi na mchana likawa linatakiwa kwenda dsm hivyo ndipo alipo anza safari,Glafla Janeth alishtuka usingizini kumbe yupo kitandani na si safarini kiukweli kabsa janeth alikua akilia na kukosa amani na kupoteza matumaini kama mfungwa aliyehukumiwa kunyongwa pale apelekwapo kitanzini,fahamu zilipo mjia janeth aligundua kuwa zile zilkjua ni ndoto tuu hivyo furaha ilitawala moyoni mwake maana usifanye masihala na kufulia ni bora tu usikie kwa jirani mtu wangu

Kindly Share This Post to sustain Mpitanjia News Blog »»

Categories:

0 comments:

Post a Comment

  • About Us

  • About Us