Monday, 21 February 2011

AMA KWELI FACEBOOK INAKOSESHA WATU AMANI

Posted by Kitalima Gerald On 05:14
 Kutokana na vishawishi vya kimapenzi kutokana na picha na meseji zinazoandikwa kwenye Facebook zimepelekea watu wengi wazisaliti ndoa zao na matokeo yake kumekuwepo na ongezeko kubwa la kuvunjika kwa ndoa chanzo kikubwa cha kikiwa ni Facebook.  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni kuhusiana na matumizi ya mtandao wa Facebook umeonyesha kuwa ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na wanandoa kuingiwa na vishawishi na baadae kuzisaliti ndoa zao kwa kuanza mahusiano ya kimapenzi na watu wanaokutana nao kwenye mtandao huo mkubwa duniani.  Utafiti uliofanywa nchini Uingereza umeonyesha kuongezeka kwa kasi ya kuvunjika kwa ndoa kutokana na watu kufumaniwa wakiwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa na watu wanaokutana nao kwenye Facebook.  Mwanasheria mmoja wa masuala ya familia alidokeza kuwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, alizisimamia kesi 30 za kuvunjika kwa ndoa na kesi zote zilihusisha mtandao wa Facebook kama chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hizo.  Mwanasheria mwengine alisema kuwa katika kila kesi tano walizozisimamia za madai ya talaka, kesi moja ilihusisha mtandao wa Facebook kama sababu kuu ya kuvunjika kwa ndoa.  Emma Patel, mwanasheria wa kampuni ya Hart Scales & Hodges Solicitors, alisema kuwa tovuti ya Facebook imegeuka kuwa mtu wa kati wa kuzitenganisha ndoa za watu.  “Facebook imekuwa ikilaumiwa kwa ongezeko la kuvunjika kwa ndoa na cha kustaajabisha katika kesi zote nilizozisimamia tangu mwezi mei mwaka jana zote zilihusisha tovuti ya Facebook kwa njia moja au nyingine”, alisema Emma.  Miongoni mwa watu waliovunjwa mioyo yao kutokana na mtandao wa Facebook ni James Wrigley, 34 wa mjini London ambaye alisema: “Mpenzi wangu alinitosa baada ya kugundua kuwa nilikuwa nikiwatumia meseji kwenye Facebook wanawake niliokuwa nikifanya nao kazi”.  “Alipata password yangu ya Facebook, alisoma meseji zangu zote na huo ndio ukawa mwisho wa uhusiano wetu wa miaka mine, sijahuzunika sana kwa sababu hatukuwa tumeoana”, aliongeza James.  Mfano mwengine ni mama wa mtoto mmoja, Marianna Gini, 32, ambaye ndoa yake ya miaka sita ilivunjika baada ya kugundua kwa kupitia mtandao wa Facebook kuwa mumewe Robert, 34, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwengine nje ya ndoa.  Mwanamke mwingine wa nchini humo aliamua kuvunja ndoa yake na mumewe baada ya kugundua mumewe alikuwa akimtumia ujumbe wa kimapenzi mwanamke mwingine ambaye hata hawakuwahi kukutana.  Msemaji wa Facebook alipoulizwa kuhusiana na lawama wanazotupiwa Facebook za kuvunja ndoa za watu alijibu kwa kusema “Ni sawa na kuilamu simu yako ya mkononi au email yako”.  “Kwani kuingia kwenye Facebook mtu hulazimishwa kufanywa kitu asichokipenda? , jibu lingekuwa ni Hapana.”, alimalizia kusema msemaji huyo wa Facebook

Thursday, 10 February 2011

HUNA SABABU ZA KUACHIKA

Posted by Kitalima Gerald On 23:09
mapenzi furaha banaa
Napenda kuwakalibisha wapenzi wasomaji wa safu hii hapa kuhusiana na mahusiano,kwani tunakuwa tukipeana elimu kwa kulekebishana ,lakini lengo letu kuu ni kuakikisha watu tunadumu na mahusiano yetu vilevile katika ndoa zetu,tukizingatia dunia kwa sasa imekua na mambo mengi yalyo na changamoto ktk maisha yetu kiujumla,jamani mwenzenu najiuliza kila siku kwanini watu wanavunja mahusianoo,ndugu yangu huna sababu za kuachika endapo utafuata haya mambo

ONYESHA KUJIAMINI
Hiki ni kipengele muhimu sana cha kwanza ambacho mwanaume wa aina yeyote anakuwa anavutiwa nacho kwa mwanamke,wanaume wengi wamekuwa wakiwajalibu wapenzi wao kwa namna moja au nyingine hasa katika zama za sasa za uwazi na ukweli,wamekuwa wakiwapa mitihani ya hapa na pale ili kuona kama anaweza kustaimili.
wanaume wengi wanaimani potofu kuwa wanawake huangalia penye pesa japo kwa namna moja au nyingine kuna uhalisia katika hali suala,huamini ni rahisi kwa mwanamke kughaili pindi agunduapo kuwa una uhusiano na mtu mwingne,mitihani hii ni kama vile kukuachia ujumbe mfupi wa kimapenzi katika simu kutoka kwa mwanamke mwingne,mwingne hutaka hata kukuonesha kuwa ana mwamke mwingne ili kukupima unajiamini kiasi gani,
sasa  basi nakushauli mwana da shostiii ambaee upo katika penzi na mtu unaempenda na sii kihisi kumpenda jitahidi kumuonesha na jinsi gani huteterreki na vitu vidogovidogo,jiamini na jifananishe na yule anayefuatwaaa utaona tafauti kubwa katika mapenzi yenuuu.
ikiwa kuna vitu anakuzidi wew zidisha majonjo kwa huyooo umpendae ,kama yeye anaumbile kubwa wewe usijali umbile lake jitume vile uwezavyo mnapokuwa faragha  na pendelea kumpa vijimaneno vya utani kuwa unajiaminii na kile alichofuata mwanzo ndicho unachojivunia nachoo hakika kama alikuwa ameenda kuonja huko nje atarudisha mapenzi yote kwako na kusahau alpo toka,
usioneshe mtu mwenye wivu kupitiliza
weka wivu wako ndani kwa ndani hata kama inaumaaa komaaa ,ikiwa huna kazi ya kufanya siku hyo tafuta kitu kitakacho kufanya uwe busy hakika utabaki katika hali yako ileile
Amini wewe ni mrembo
amini wew ni mrembo na ndiyo maana alikuchagua wewe na sii mtu mwignee,kama yeye alikufuata tena huku akitilia huruma anaitaji kuwa na wew kwa nguvu zake zote basi hakukosea njia hapo ndipo mahali pake,atajifanya anakusaliti lakini tambua hyoo ni tamaa yake tuu kwani kila kitu kizuri kwa moyo wake anakipata kutoka kwako na sii sehemu nyingne baki,najua inauma lakini wewe kuwa mvumilivu kwani itafika mahali yeye atagundua anahangaika ila mambo yote mazuli yako nas wewe,wahenga wanasema mvumilivu hula mbivuuuu,
KUWA MWELEVU!
Mwanaume wa sasa anataka mwanamke aambaye ana uelewa mkubwa wa kufikili na kutafakari mambo na sii mwanamke anaye kulupuka kwa kufanya maamuzi,au katika kufikili jambo mwanaume aliye makini huaanza kuangtali hili suala pale usiano tu unapo anza ,akisha gundua kuwa ulewa wako ni mdogo hata weza kudumu nawe kwani atatafuta sababu ili tu kuvunja uhusiano kwani anaona utampa shida mbeleni,na hili nlimewakuta wengi mtu anaanza kusema kuwa flani amebadilika ,ukiona hivi jua lazima kuna tatzo huenda umekua na uwezo mdogo wa kutaza mambo ,au unamshauri vitu ambavyo hakutegemea kuvisikia kutoka kwako tena bora viwe vya muhimu hapo mtaernda sawa 
USIMTEGEMEE SANA!
Kama mwanamke usimtegemee mwanaume katika kipato moja kwa moja kwani kwa kufanya hvyo utakua mzigo kwake hvyo kwa namna moja utakuchoka kwa haraka sana,wanaume wa sasa wanataka wanawake ambao  watasaidiana kuendesha gurundumu la maendeleo,ili kupunguza ukali wa maisha ikitokea unataka kumtegemea kwa kila kitu unaongeza ukali wa maisha kwake,hvyo atashindwa kuendelea na wewe. 
Mwache mwanaume wako atafute pesa za kujenga maisha yenu wewe pamoja na watoto baadea na si kutafuta pesa za kuku honga wewe ,jua atakubali kukuhonga kwa kuwa anakupenda  na hapendi kukupoteza sasa jiulize akipata mtu akimuonesha mapenzi zaidi tena bila hata kuhongwaa werwe utakua wapi?
       
  • About Us

  • About Us